MIMI MWENYE HATIA
145
Wokovu No 2911 Mimi mwenye hatia
Nilikombolewa,
Mwokozi alipojitoa.
Zambi zangu na
zako alizichukua,
Kwa damu aliniokoa.
Zambi zimetungikwa
msalabani Alipojitoa,
Mwokozi. Alizarauliwa
na kukataliwa
Atupatanishe na Mungu.
2 Yesu mwenye upole
na mwenye upendo
Ananitakasa rohoni.
Nimepata uhuru kwa
Yesu Mwokozi,
Alikufa msalabani.
3 Namwambata Mwokozi,
sitaki kumwacha,
Kwa kuwa alinifilia.
Nakusifu, E’Yesu,
unayenipenda,
Daima nakushangilia.