E’MUNGU MWENYE HAKI
144
Wokovu No 2751 E'mungu mwenye haki
Uniongoze huku
Katika mambo yote
Yanayokupendeza!
Nikiwa huku bila
Wewe, Vitisho,
hofu na mashaka
Yatanitia tetemeko
mpaka kufa.
2 Ni heri siku zote
Kutegemea Yesu Na
kutembea sawa
Katika nyayo zake,
Kwa kuwa Yeye
ni Mchunga
Anayeniongoza vema,
Nipate kuingia
katika raha yake.
3 Safari yangu sasa
Yaelekea mbingu,
Mwokozi yuko huko,
Lazima nifikeko Na
siku nitakapofika
‘tashangilia kwa
furaha Kuona Yesu
aliyeninunua kwake.
4 Ulimwenguni humu,
Matata na kuchoka.
Nikihitaji kitu
Nafazaika bure,
Lakini siku ile kuu
Nita’pomwona Mkombozi,
Natumaini sitakosa
zawabu yangu!
5 Mbinguni sitaona
Adui zangu tena.
Hayatakuwa mambo
Yakupokonya pale.
Sauti nitamtolea,
Kusema: Mungu,
Haleluya! Mikono
nitaipepeya kwa
shangwe kuu !