NJOO KWA YESU MWOKOZI
140
Wokovu No 2021 Njoo kwa Yesu mwokozi
Unayeteswa rohoni!
Daamu iliyomwagika
itakuosha kabisa.
Njoo kwa Yesu
Mwokozi, Naye
atakuokoa!
Ulimwenguni
ni dhiki, Kwake
ni raha halisi.
2 Mbona kukuwa zambini
Bila uzima wa
Mungu? Uje upesi
kwa Yesu Ili
upate amani !
3 Saa zapita upesi,
Hazitarudi kabisa.
Bado kidogo na tena
Utapelekwa kuzimu.
4 Yesu atamchukua
Bibi-Arusi mbinguni,
Na tutaimba milele
Sifa za Mwana-Kondoo.
Huko karibu na
Yesu, Mbali ya
mambo ya nchi,
Huru na heri rohoni
Nitafurahi milele!