MWENYEZI MUNGU ANAFANYA
141
Wokovu No 2151 Mwenyezi Mungu Anafanya
Ishara kubwa duniani,
Anaondoa minyororo
Inayofunga watu huku.
Avunja nyavu za
Shetani, Na
wakosaji waokoka.
2 Maneno yake yana
nguvu, Kushinda
yote ya zamani.
Na watu wanapiga
mbio, Kuomba ne’ma
ya Mwokozi. Wakiyapata
masamaha, Waimba
wote: “Sifu Mungu!”
3 Tazama, ndugu wengi
sana, Wanafuata Yesu
leo; Katika kila
inchi sasa Maelfu
wanapenda Mungu.
Wengine wanavutwa
naye Mwenyezi
Mungu, Baba yetu.
4 Inua macho, mvunaji,
Mavuno yanaivya
sana! Uende
kutafuta watu,
Uwapeleke kwake
Yesu ! E’ndugu
wote amkeni,
‘kawaokoe wenye
zambi !
5 Wengine wanapoingia
Ufalme wako Yesu
Kristo, Nisibakie
huku chini, Neema
hiyo nakuomba !
Nakaa mikononi
mwako, Unifikishe
huko kwako !
6 Najua siku ni
karibu, Mwokozi
atakaporudi,
Awachukue watu
wake, Mpaka nchi
ya amani. E’siku
ya uheri bora,
Nakutamani Uje mbio!