E’RAFIKI SHAKA ZAKO
138
Wokovu No 154
1 E'rafiki shaka zako
Zipeleke kwake Yesu!
Aliyemwamini Yeye
Hataona haya kamwe.
 
Naamini, Naamini,
Ninakuamini, Yesu.
Naamini, Naamini,
Naamini Neno lako.
 
2 Zambi zote ziungame
na kwa damu utakaswe,
Akuvike haki yake!
Atakusafisha kwake.
 
3 Masumbuko yako yote
Uyalete mbele yake!
Ukipita uvulini,
Bwana Yesu yupo nawe.
 
4 Na furaha yako pia
Ijulishe kwake Yesu,
Yeye Bwana ju’ya
yote, Akubarikie yote!
 
5 Ujitoe kwake Yesu:
Roho, Mwili na
Akili ! Vyote vya
maisha yako
Anataka ku’takasa.