NAONA PENDO KUBWA MNO
134
Wokovu No 124
1 Naona pendo kubwa
mno Latoka kwa
Mwokozi wangu, Ni
tele kama maji
mengi Yatembeayo
baharini. Lanitolea
tumaini Ya kwamba
nitatiwa nguvu;
Na niwe mhodari
tena Kwa pendo
kubwa la Mwokozi !
 
Haleluya !
Ni pendo kubwa
Linalotoka moyo
wako ! E’Mungu
wangu, nakuomba
Nijaze pendo
lako tele !
 
2 Na pendo hilo kubwa
mno Huyaondoa majivuno,
Na kunifunza haki,
kweli, Uongo wote
niuvue! Hunituliza
moyo wangu, Huruma
nayo hunitia. Na sote
tuwe na umoja Katika
pendo la Mwokozi !
 
3 Nijazwe pendo hilo
kubwa, Linibidishe
siku zote! Rohoni
niwe na juhudi
Nitumikie Bwana
Yesu! Hazina yako
ni’peleke Kwa
watu waliopotea,
Wafahamishwe
pendo kubwa Ulilo
nalo, Mungu wangu !