HERI HALISI
135
Wokovu No 143
1 Heri halisi Yesu
ni wangu ! Yeye
Mchunga, mimi ni
wake. Heri yakini,
yote ni heri,
Roho na moyo
zimeokoka.
 
Yesu ni wimbo
na raha yangu,
Nitamsifu hata
milele !
Nanitamwona
huko mbinguni.
Yesu ni wangu,
nami ni wake.
 
2 Nikijitoa kwa Bwana
Yesu, Na nilipewa
wokovu wake. Huko
mbinguni kuna furaha
Juu ya mtu aliyetubu.
 
3 Sasa naweza kusifu
Yesu, Na roho yangu
inafurahi. Mimi si
kitu mbele ya
Mungu, Bali ni
heri, Namshukuru.
 
4 Nimebatizwa katika
Roho, Shangwe ya
mbingu imo rohoni.
Moto moyoni, pia
kinwani, Nashuhudia
pendo la Mungu.