NILIPOFIKA GOLGOTHA
132
Wokovu No 117
1 Nilipofika Golgotha
Nikaiona huko Neema
kubwa kama mto,
Neema ya ajabu.
 
Neema ya Golgotha
Ni kama bahari
kubwa, Neema tele
na ya milele,
Neema ya kutosha !
 
2 Nilipofika moyo
wangu Ulilemewa sana,
Sikufahamu bado vema
Neema yako kubwa.
 
3 Nilipoona kwamba
Yesu Alichukua zambi,
Neema ikazihirika,
Na moyo ukapona.
 
4 Mbinguni nitakapofika,
Furaha itakuwa Kuimba
juu ya Neema,
Milele na milele.