NINA UZIMA WA MILELE
131
Wokovu No 78
1 Nina uzima wa
milele Na tumaini
ni imara, Mbingunu
tutaona Yesu,
Mwokozi wangu,
kwa furaha.
 
2 Nina uriti bora
huko, Unaolindwa
hata mwisho. Na
kila siku ya jaribu
Natiwa nguvu
naye Baba.
 
3 Namshukuru Mungu
wangu! Ananitunza
siku zote. Katika
shida na taabu,
Kwa hiyo sisumbuki tena.
 
4 Rohoni mwangu ni
amani, Naimba kwa
furaha kubwa.
Nikiongozwa naye Yesu
Naendelea kwa salama.
 
5 E’Bwana Yesu,
unifunze ku’tumikia
Wewe vema. Wakatu
ubakio tena Wa mwendo
wangu duniani.