DAMU YAKO YENYE BARAKA
124
Wokovu No 10
1 Damu yako yenye
baraka Inayotuosha
makosa, Ilitoka
msalabani, Bwana
Yesu, ulipokufa.
Nastahili ‘pata
hukumu, Na siwezi
mimi kujiosha.
Unioshe katika damu,
Nipate kuwa
safi kabisa !
 
Safi, safi kweli,
Safi, safi kweli !
Unioshe katika damu,
Nipate kuwa
safi kabisa !
 
2 Yesu, ulivikwa miiba,
kutungikwa juu ya mti;
Ulivumilia mateso,
maumivu na majeraha;
ninataka kijito hicho,
n’ende na nikasafishwe
sana ! Unioshe katika
damu, nipate
kuwa safi kabisa !
 
3 Baba, kweli nina makosa,
moyo wangu wa uzaifu;
Mimi mwenye zambi rohoni
Nitaona wapi Mwokozi ?
Yesu kwako msalabani
Naja ninakuamini sasa.
Unioshe katika damu,
Nipate kuwa safi kabisa !
 
4 Bwana nimefika karibu,
unilinde kwako milele !
Ufungue kila kikamba
Unijaze moyo mwenyewe !
Na karibu na msalaba,
Nitakaa hata kufa
kwangu. Unioshe
katika damu, Nipate
kuwa safi kabisa.