JUU YA MBINGU ZOTE
125
Wokovu No 211 Juu ya mbingu zote
Nyota na jua pia,
Hapo yafika kweli
Maombi ya wenye dua;
Roho ya mwanadamu
Yamfikia Mungu,
Huko yabisha lango
Na kumtafuta Baba.
2 Roho haitaona Raha
amri huku ; Kuna
bandari njema Mbinguni
kwa Mungu Baba.
Moyo utatulia, Nuru
itatokea Tukitafuta
njia ya sala na maabudu.
3 Hata mtoto ‘dogo,
Mwenye kuomba Mungu,
Hana la kuogopa;
Kuomba kwafaa sana.
Tusisahau tena, Pote
twendapo huku Kwamba
maombi yetu Yafika
kwa Mungu Baba.