DUNIA SI KWETU
68
.1 Dunia si kwetu,
Mimi ni msafiri.
Ninayo lazima mbinguni
kwa Baba. Mulango
ni wazi mbele
ya malaika, Na
sitaikumbuka dunia milele.
Mwokozi wajua,
Sina rafiki kama
wewe. Ikiwa mbinguni
siwezi kuingia, Bwana
nifanye je hata
nikae nawe? Na
sitaikumbuka
dunia milele.
2 Tuishi milele mbinguni
kwa Bwana. Wimbo wetu
huo, Uimbwa na washindi.
Tutaimba sifa zake na
utukufu, Na sitaikumbuka
dunia milele.
3 Wajua waningojea,
Ulivyo nijuavyo,
Nimeokolewa sasa,
nipo tayari. 'Najua
nitafika ingawa ni
m’nyonge, Na
sitaikumbuka dunia milele.