UKAE NAMI
69
.1 Ukae nami, Giza
inafika. Usiniache,
Mungu, 'Nakuomba.
Unayeweza uzaifu
wangu. 'Nategemea
wewe. Ukae nami.
2 Maisha yangu ni
mafupi sana. Uzuri
wa dunia Utakwisha.
Kuna machozi, Kufa
huko chini. Wewe
Mwokozi wangu,
Ukae nami.
3 'Nakuhitaji wewe
siku zote. Unayeweza
sana kunilinda. Wewe
shujaa wa kushinda
wote. Katika hali
zote, Ukae nami.
4 Unionyeshe musalaba
wako. Nione nuru
yako kati giza.
Na nikiishi ao
nikikufa, Wewe
Mwokozi wangu,
Ukae nami.