MWOKOZI WANGY NI MWAMBA BORA
148
Wokovu No 237
1 Mwokozi wangy ni mwamba
bora Ahadi kama milima;
Zaniletea Amani tele,
Na mibaraka daima.
Katika mwamba ni raha
kuu, Baraka tele kutoka
juu. Nakaa humo,
ninastarehe, Ni
heri sana milele.
 
2 Makimbilio ni mwamba huo
Katika teso lo lote;
Nisikimbie adui ‘kuu,
Nishinde katika vyote!
Dunia yot’ ikitingizika,
Ahadi zake hazipunguki.
Nakaa humo, ninastahere,
Ni heri sana milele.
 
3 Nakaa mbali ya udhalimu,
Hatia, dhambi, hukumu.
Na kwa Imani nikisimama,
Adui anakimbia. Nayo
mawazo ya giza tupu
Hayatapata nafasi huko.
Nakaa humo, ninastarehe,
Niheri sana milele.
 
4 Nafurahia Baraka zote
Za ulimwengu wa roho.
Karama hizo nalizipewa
Katika kufa kwa Yesu.
Hakuna woga na shaka
huko, Hayatakuwa
manunguniko.
Nakaa humo,
ninastarehe,
Niheri sana milele.