KWA SALAMA BABA MUNGU
128
Wokovu No 52
1 Kwa salama Baba Mungu
Awalinda watu wake, :/:
Hata nyota za mbinguni
si salama kama wao :/:
 
2 Mungu awalinda hivyo
Katika upendo wake :/:
Wanakubaliwa naye,
Wanarehemiwa sana :/:
 
3 Hawavutwi toka kwake
Kwa furaha wala shida :/:
Yeye ni rafiki ‘kubwa
Wa walio watu wake :/:
 
4 Wanalishwa, wanavikwa,
Wanafarijiwa naye :/:
Hata nwele za kichwani
zimehesabiwa zote :/:
 
5 Enyi kundi lake ‘dogo
Mungu atawakingiza ! :/:
Na adui watashindwa
Kwa uwezo wake ‘kubwa.
 
6 Akitoa, akiwapa, Baba
yenu hageuki. Na mapenzi
yake ndiyo :
Wana wapatishwe wema.