A’MENIWEKA HURU KWELI
127
Wokovu No 40
1 A'meniweka huru kweli
Naimba sasa Haleluya!
Kwa msalaba nimepata
Kutoka katika utumwa.
 
Nimeokoka, nafurahi!
Na zambi zangu
zimetoka. Nataka
kumutumikia Mwokozi
wangu siku zote.
 
2 Zamani nilifungwa
sana Kwa minyororo
ya Shetani,
Nikamwendea Bwana Yesu,
akaniweka huru kweli.
 
3 Neema kubwa !
Nilipata Kuacha njia
ya mauti, Na nguvu
ya wokovu huo,
Yanichukua siku zote.
 
4 Na siku moja
nitafika Mbinguni
kwake Mungu wangu.
Milele ninamhimidi
Na kumwimbia
kwa shukrani.