SIKU MOJA BARAGUMU
65
.
1 Siku moja baragumu,
Yake Mungu italia.
Bwana Yesu atashuka,
Kuwatwaa watu wake.
 
Siku Yesu atakuja,
Nitakwenda kwake juu,
Aleluya, Nitamuimbia
kwa furaha,
Siku Yesu atakuja.
 
2 Na Wakristo wengi
sana, Walitangulia
mbele. Watafufuliwa
kwanza, Siku
Yesu atakuja.
 
3 Ee, rafiki, siku ile,
Usipokuwa tayari.
Utabaki hapa chini,
Siku Yesu atakuja.
 
4 Uje sasa kwake Yesu,
Atakuokoa leo.
Utakuwa ku safari,
Siku Yesu atakuja.