'NATAKA KWELI KUJONGEA
33
.
1 'Nataka kwelt kujongea
kwako Bwana Yesu.
Uliyeniokoa nami
ninakuwa wako. Kwa
nguvu yangu yote
nitafuata njia yako.
Na leo ninataka
kujongea kwako Bwana.
 
Karibu kwako Bwana,
karibu kila siku.
Karibu Bwana Yesu,
Nijongee kando yako.
 
2 Uliyejaribiwa na Shetani
ku jangwani. Kwa nguvu
yako peke uliweza
kumushinda. 'Naomba
nguvu ya kushinda
majaribu yake. Na
leo ninataka
kujongea kwako Bwana.
 
3 Zamani watu wako
walikukimbia pia.
Walikuacha kwenda ku
hukumu peke yako. Kwa
kukufuata mbali woga
uliowashika. Na
leo ninataka
kujongea kwako Bwana.
 
4 Maneno ya dunia na
tamaa zake zote,
Ninaziacha pia kwa
kukujongea Bwana. Maneno
yako peke yanajaza moyo
sasa. Na leo ninataka
kujongea kwako Bwana.
 
5 Na siku moja utakuja
kuwatwaa wako, Walio hai
na walio wafu wataitwa.
Sitaki kubakia ku Safari
yako juu. Milele ninataka
kuikaa kwako Bwana.