HERI KWAKE
32
.
1 Heri kwake anayeamini,
Mungu Baba na Yesu Mwokozi.
Heri kwake anayeifuata,
Njia nzuri iendayo mbinguni.
 
Sifa kwako, Yesu Kristo,
Unakuwa Mwokozi kabisa.
Sifa kwako, Yesu Kristo,
Uso wako 'taona mbinguni.
 
2 Ni vizuri kufika pamoja,
Kusikia maneno ya Mungu.
Kule mbingu karibu naYesu,
Tutaona furaha kabisa.
 
3 Kuamini pasipo kuona,
Ni vizuri katika safari.
Siku moja atakaporudi,
Tuta’kaa milele mbinguni.
 
4 Watu wengi wangali ku giza.
Hawajui njia ya mbingu.
Twende sasa kuwaionyesha,
Na wafike pamoja na sisi.