NI HERI KUONA NDUGU NJIANI
29
* Wokovu No 60
1 Ni heri kuona ndugu
njiani pa kwenda mbingu.
Tukinyong’onyea sana
kwa kuwa tu peke yetu,
Kushirikiana kwa ndugu,
Kunaturudisha moyo;
Na Mungu atupa nguvu,
Tukiyainua macho.
 
2 Twafungamana rohoni,
Tulio wa nyumba yake,
Huoni ulimwenguni,
Kushirikiana kwetu.
Na tuna Mwokozi mmoja,
Imani ni moja pia,
Watoto wa Baba 'moja,
Twashika sheria yake.
 
3 Furaha ya ulimwengu,
Haitatuvuta tena,
Twaona kung’aa kwake,
Ni bure na bila kisa.
Lakini tukikusanyika,
Kwa jina la Mungu Baba,
Atuandalia kweli,
Karamu iliyo bora.
 
4 Tukivumilia hata,
Ukomo wa mashindano,
Mbinguni tutawaona,
Wakristo wapenzi wote.
Hatutatawanyika huko,
Tu wote umoja kweli,
Milele tuta’pokaa
Nyumbani mwa Baba yetu.