'NAIAMINI DAMU YAKO
28
Wokovu No 9
1 Naiamini damu yako
na msalaba wako, Yesu.
Mwokozi wangu wa pekee,
'napata yote kwako.
 
Uliyoyaahidi
'napata kwa imani.
Huwezi kuniacha mimi;
'napata yote kwako.
 
2 Kwa damu nimetakasika,
na mto wa uzima wako,
waniletea nguvu tele,
'napata yote kwako.
 
3 'Nafungwa kwa upendo
wako, njiani unaniongoza,
na katika hatari zote,
'napata nguvu kwako.
 
4 Ninakupenda, Bwana
Yesu, wanisikia niombapo,
wanipa jibu la maombi,
'napata yote kwako.