NILIOKOLEWA NA YESU
23
. 1 Niliokolewa na Yesu,
Kwa damu iliyomwangika.
Alinilipia makosa,
Aliniokoa kwa kifo.
Wokovu wa Yesu,
Aliniokoa kabisa.
Wokovu wa Yesu,
Na mimi ni wake milele.
2 Niliokolewa na Yesu,
Furaha ya mbingu moyoni.
Na ninamwimbia Mwokozi,
Alinikomboa kabisa.
3 Niliokolewa na Yesu,
Uzima ninao moyoni,
Uzima ule wa milele,
Ni wangu kwa pendo la Yesu.
4 Niliokolewa na Yesu,
Kusifu siwezi kuacha.
Pamoja na waaminifu,
Milele nitamushukuru.