YESU AMENIOKOA
22
Wokovu No 361 Yesu ameniokoa,
amenipa utulivu.
Kwake ninaona raha,
Ninataka kumsifu.
Haleluya, Haleluya!
Nimefika bandarini.
Haleluya, Haleluya!
Jina lake Yesu ni munara.
2 Kwa furaha ninaimba,
Wimbo mpya wa wokovu.
Nisichoke kamwe hapa,
Kumwimbia Mkombozi!
3 Ni habari za neema,
Za kupasha pande zote.
Mhubiri, Enda mbio,
Kufikia nchi zote !
4 Yesu, siku nita’kufa,
Na maisha ni tayari,
'Nichukue kwako juu.
Penye raha ya milele !