SAWA NA KISIMA SAFI
19
Wokovu No 1441 Sawa na Kisima safi,
Chenye maji mengi mema,
Ni upendo wa mwokozi,
Ukaao ndani yake.
Yesu amelifungua,
Lango zuri la mbinguni,
Ili niingie humo
kwa neema yake kuu.
2 Kama ndege awindavyo,
Mara nyingi nili'umwa,
Moyo wangu ulilia,
Yesu hakunifukuza.
3 Ni ajabu kubwa kweli,
Alinisamehe yote !
Juu ya rehema yake,
Ninaimba kwa furaha.
4 Asubui ya uzima,
Nitafika mlangoni;
Kwa ajili ya upendo,
Nitapata kuingia.