TUMEPATA NENO NZURI,
18
.
1 Tumepata neno nzuri, Yesu
alituokoa. Tulipashe kwa wengine
Yesu alituokoa. Linafaa kusikia
kwa wazee na watoto, Ni habari
ya furaha, Yesu alituokoa.
 
2 Tuna hamu ya kuimba, Yesu
alituokoa. Ni hukumu ya makosa,
Yesu alituokoa. Kweli alitufungua,
Alivunja minyororo. Atatuhamisha
kwake, Yesu alituokoa.
 
3 Neno kubwa la ajabu, Yesu
alituokoa. Juu ya mashida yote,
Yesu alituokoa. Sema nikingali
hai, Imba nikatapo roho. Ninataka
kusikia, Yesu alituokoa.
 
4 Wote wasikie wazi, Yesu
alituokoa. Inchi zote zifurahi,
Yesu alituokoa. Siku za furaha
ile, Watu watajua wazi, Tuliimbe
na furaha, Yesu alituokoa.