KWA PENDO LAKE KUBWA
10
.
1 Kwa pendo lake kubwa,
Aliponitafuta.
Akanitosha mimi ku
njia ya mabaya. Na
nyimbo za malaika wengi
zikajalisha mbingu pia.
 
Akanitafuta, Akaniokoa,
Akaniondosha kwa mabaya.
Ninakuwa mutu wake sasa.
 
2 Muchunga mwema Yesu,
Akaniponya roho.
Aliponiambia,
Mutoto nakupenda.
Sauti yake ya mapendo
iliyonifariji sana.
 
3 'Naona damu yake
itokayo vidonda.
Na taji ya miiba,
mateso na mauti.
'Nataka kushukuru Yesu
karibu musalaba wake.
 
4 Ninamufuata Yesu
kwa nuru yake sasa.
Mapendo yake Mungu
ya’pamba njia yangu.
Miaka yote itafaa
kusifu Yesu kwa furaha.
 
5 Na saa zinapita,
nangoja asubui.
Utakaponiita niende
kwako juu. Nitasimama
kwa amani mbinguni
mbele macho yako.