YESU ANAPITA NDUGU
120
.
1 Yesu anapita ndugu
Na rafiki za dunia.
Kwa maisha yangu yote,
nikufuate tu karibu.
 
Nikufuate wewe,
Yesu,
Nikufuate wewe,
Yesu.
Kwa maisha yangu yote,
Nikufuate tu karibu.
 
2 Sitamani mali tena,
Wala sifa na heshima.
Kitu hiki ninataka,
Nikufuate tu karibu.
 
3 Hata unaniongoza,
Kwa mateso na huzuni.
Nitafika siku moja,
Kupumzika kwako Yesu.