NILIKWENDA MBALI SANA
81
.
1 Nilikwenda mbali sana,
Kuifuata njia mbaya.
Nikamusahau Yesu,
Aliyenipenda kweli.
 
Nina raha na furaha,
Yesu alinitafuta.
Akaniokoa kweli.
Mimi wake kwa milele.
 
2 Na sikufikiri kwamba,
Nitakapokusimama,
Mbele yake Mungu tena,
Siku ya hukumu kubwa.
 
3 Zambi zilinichokesha,
Nikamuendea Mungu.
Akasema neno zuri,
La amani na furaha.
 
4 Niliomba Bwana Yesu,
Anijaze Roho yake.
Nipate kushinda kweli,
Majaribu ya Shetani.
 
5 Siku Yesu atarudi,
Kuwatwaa watu wake,
Nami nitakwenda naye,
Ku safari yake juu.