NJOO KWA YESU !
78
.
1 Njoo kwa Yesu!
Usikawie, Atuonyeshe
njia kwa wazi.
Anaikaa hapa pa kati,
Akinongona, "Njoo!"
 
Njoo sasa kwake
Bwana Yesu!
Atakuokoa kwa mabaya.
Atakusaidia utubu,
Ukageuze moyo.
 
2 Yesu a'ita watu
wo wote. Anawapenda
wapoteao. Wenye
masikitiko na kazi,
Waje kupumuzika.
 
3 Tena nafasi leo ya
kuja, Kwake Mwokozi
tufunguliwe. Leo
tutubu, tusamehewe,
Tuondolewe zambi.
 
4 Saa z'ataka kwisha
upesi. Yesu a'ngoja,
tumuamini. Shika
furaha, pata uzima,
Sasa usikawie.