KAMBA ZA MAUTI
60
.1 Kamba za mauti
zimenizunguka, Kuuma
kwa kaburi, Kumenishika
sana, Uchungu wa kufa
hauna mwisho, O!
Mimi nimechoka na
kulia kwangu. Ona
shingo langu,
Limenikauka. Ona
macho yangu, Ya'ona
ningali. Tena macho
yangu ya'ona ningali.(x2)
Mimi 'nangojea,
O! O! Mungu wangu.
2 Mimi nimezama kati’
matope mengi. Kule maji
mengi yamenigarikisha.
Kule nilikuta
huzuni na taabu.
3 Pale unaenda, Pale
hakuna kitu, Wala
ufahamu na wala
maarifa. Ulifanya
vyote wakati wa ujana.
4 Ulitoka mavumbi, Utarudi
mavumbi. Ulikuja
utupu na utarudi utupu.
Ili kila andiko,
O! Litimie.
5 Ndugu, Ukiamini,
Ukisha kuamini,
Ukisha kuamini,
Unatambuka mauti,
Unatambuka mauti,
Na kuingia uzima.