MAISHA KATIKA DUNIA
58
.
1 Maisha katika dunia,
Ni kama kupanda na
vuna, Apandaye katika
Mwili, Atavuna uharibifu.
Tukitumikia Mwokozi,
Tutapata zawabu mbinguni.
Yafaa kuishi na kufa
katika maneno ya Mungu.
 
2 Kwa neema kubwa kabisa,
Tumekubaliwa na Mungu,
Kwa neema kubwa zaidi,
Twapata kumutumikia.
Kuishi kwa jili ya Yesu,
Kati yote ya dunia hii,
Na kuitangaza Injili,
Ni faida kwetu kabisa.
 
3 Wakristo wata’poingia,
Mbinguni kusifu Mwokozi,
Na mimi nataka kufika
kuimba pamoja na wao.
Tutamushukuru Mwokozi,
Aliyetununua kwa Damu,
waliohudumu kwa pendo,
watamuhimidi milele.