E'YESU INGIA ROHONI
40
.1 E'Yesu ingia rohoni kabisa,
Uniweke huru na kunitakasa.
Nipate kushirikiana na wewe,
Katika mateso na raha daima.
Ee, Bwana, nijaze upendo
wa mbingu nao utabiti,
Niwe mushindaji. (x2)
2 Siombi ufalme, Siombi
heshima, 'Naomba kupewa
neema daima, Nijue yakini
ya Neno la Mungu: Mtoe
miili na iwe zabihu.
3 Nishike rohoni, unichungulie,
Na katika yote unisaidie,
Nipate kabisa kusudi na nia
kujitoa kwako, kukutumikia.
4 Hakuna la huku litanizuia,
Nisilingamane na Yesu Masiya.
Nitumaini je kufika mbinguni
Nisiposhiriki Mwokozi mpendwa ?