SAUTI YAKE BWANA
37
.
1 Sauti yake Bwana ikamujia
Yona kuwahubiri Waninawe.
 
Shetani 'kamuingia Yona
upesi sana 'kasema:
"Kimbilia mujini Tarasisi."
Yona akapanda katika mashua,
Akafika katikati ya bahari,
Mungu naye akatuma mawimbi.
Tazama, kilio kikafika,
wakatupa Yona baharini.
Samaki akamumeza.
 
2 Yona alilala ndani ya
samaki muda wa siku tatu, akiomba.
 
3 Mwisho wake Yona alikubali
kwenda kuwahubiri Waninawe.
 
4 Ee, wee mwenzangu nawe, uwe
tayari kwenda kuwahubiri mataifa.