WALIKOMBOLEWA WAIMBA JUU
25
Wokovu No 307
1 Walikombolewa waimba juu,
Wakisujudu mbele zake Bwana.
Huzuni na taabu zake dunia
Bwana amewaondolewa zote.
 
Wanamuimbia Mwana
Kondoo aliyekufa,
Sasa yu hai,
Ameyashinda mauti.
 
2 Wanashika vinumbi mikononi,
Wakiimba wimbo wa Mwana Kondoo.
Na Musa mtumishi wake Mungu,
wakifurahia kushinda kwake.
 
3 Wasiopenda kumsujudia,
Katika dunia hii ya sasa.
Hawataonekana mbele zake,
Watateketea motoni kweli.
 
4 Muda unaobaki ni mfupi,
Tujitayarisheni ndugu sasa.
Bwana ajapo tuwepo tayari,
tutaimba naye kule mbinguni.