UZIMA NINAO
16
. 1 Uzima ninao moyoni daima,
Uzima ni Yesu Mwokozi.
Niliyezaliwa na roho ya
Mungu,'Napata uzima wa Yesu.
'Nashiba rohoni na
raha ya Mungu, Na
moto wa mbingu ulimo.
'Napata kukaa nuruni
kabisa, Na nuru
ni Yesu Mwokozi.
2 Vilivyo katika wokovu wa
Yesu, Aliyenifia zamani.
Nikimuamini Mwokozi najua,
Ataniokoa kabisa.
3 Aliniokoa katika mauti,
Na sasa 'napata uzima.
Furaha moyoni ninamwimbia,
Mwokozi anayenipenda.
4 Furaha zaidi kuona
wengine, Wanaomwamini Mwokozi.
Wapate wokovu, uzima,
furaha, Tufike pamoja mbinguni.
5 Maisha mazuri kabisa
'naona, Ananiongoza njiani.
Furaha na wema 'napata kwa
Yesu, Mwokozi anayenipenda.