MATENDO YA MUNGU
14
.
1 Matendo ya Mungu
ya’pita fahamu.
Ni nani hajaona wazi?
Lakini 'najua maneno
ya Mungu kwa mimi
ya'faa kabisa.
 
2 Njiani sijui maana
yo yote, Lakini
nitayafahamu.
Kwa nini kujisumbukia
kwa bure, Taabu
na shida za muda.
 
3 Wakati wa giza,
pasipo kuona, Nitamuamini
Mwokozi. Aliyenifia,
ataniongoza,
Nifike salama mbinguni.
 
4 Na kama Elia,
upesi kabisa,
Nitakapoacha dunia.
Uchungu na shida
za huku takwisha.
Milele nitashangilia.
 
5 Tutamuabudu Mwokozi
daima, Kuimba,
kusifu milele.
Ee, Mungu wa haki
na mwenye rehema,
kwa vyote unatutendea.
 
6 Halafu 'nangoja
kwa uvumilivu,
Kujua maana kwa wazi.
Na'lo tumaini ni
lenye uzima,
Uriti ninao mbinguni.