NURU IKIFIKA
8
.
1 Nuru ikifika,
Giza l’akimbia.
Nuru yetu ndio Yeye,
Yesu Mukombozi.
 
Tumusifu Yesu,
Tumusifu sana.
Sifa zake tusichoke.
Alitukomboa.
 
2 Siku moja Yesu
atakuja tena,
Kuwatwaa watu wake,
Atawapeleka.
 
3 Watu wa Shetani
watatangatanga,
Hata giza la Shetani
litawafunika.
 
4 Watu wengi sana
watalialia. Watasema,
“Yesu, Bwana,
utufungulie.”
 
5 Bwana Yesu naye
atawaambia, “Ondokeni!
Siwajui hata mutokapo.”
 
6 Watu wa Masiya
watafurahiwa,
Na furaha ya mbinguni
hata kwa milele.