'NAONA MAAJABU
6
.1 'Naona maajabu leo
(Yatoka),
Yatoka Bwana Mungu wetu
(Wa kweli).
Katika ahadi zake
(Ishara),
Ishara imeonekana
('Naona).
'Naona maajabu kubwa
('Napenda),
Napenda kushukuru Mungu.
(Kwa nini ?)
Kwa kuwa a’nipenda mimi
(Ishara)
Ishara kubwa toka Mungu.
2 Katika duniani yote
(Ni mambo)
Ni mambo mengi ya ajabu
(Ni Yesu).
Ni Yesu a’wapita wote
(Kufanya),
Kufanya maajabu mengi
('Naona).
3 Ni kama tetemeko kubwa
(Kabisa),
Litembealo ndani yangu.
(Ni kiku-)
Nikikumbuka Yesu Kristo
(Ya kuwa),
Angali a’nipenda mimi
('Naona).
4 Viziwi na viwete vyote
(Na bubu),
Vipofu na wakoma wengi
(Vilema),
Na wafu walifufuliwa
(Kwa jina),
Kwa jina lake Yesu Kristo
('Naona).
5 Mapendo yake Mungu kwangu
(Makubwa),
Yananijaza roho tele
(Upendo),
Upendo wake Yesu Kristo
(Ni dawa),
Ni dawa manukato kwangu
('Naona).
6 Kwa mulima wa Mizeituni
(Twaona),
Angaa uso na mavazi.
(Tazama!)
Tena kutembea kwa maji
(Ishara),
Ishara imeonekana
(Sauti).
Sauti ya Mungu ya'sema
(Ni huyu)
Ni huyu Mwanangu mupendwa.
(‘Napendezwa)
'Napendezwa na kazi yake.
(Sikieni)
Sikieni maneno yake.
('Naona).