NIMEFIKA KWAKE YESU
4
.
1 Nimefika kwake Yesu,
Na kwa roho yangu sasa.
Jua lake la neema,
Linangaa kila siku.
 
Roho yangu inaimba,
Nimefunguliwa kweli.
Nimekaribia Yesu,
Ninaimba kwa furaha.
 
2 Pepo za neema yake,
Zinavuma ndani yangu.
Na furaha ya wokovu,
Inanijalisha tele.
 
3 Sasa Yesu peke yake,
Anakaa kwangu kweli.
Nimepewa mufariji,
Roho ya ahadi yake.
 
4 Siku Roho afikapo,
Mutajua wazi wazi, Mimi
nitabaki kwenu,
Hivyo Yesu alisema.
 
5 Kweli amefika kwetu,
Sasa yupo hapa nasi.
Tujitoe kwake Mungu,
Azioshe roho zetu.
 
6 Yesu atakaporudi,
Na katika utukufu, Mimi
nitamufanana,
Nitamushukuru sana.