SITASUMBUKA
2
.
1 Sitasumbuka kwa kuwa
Mungu a’nitazama kwa vyote.
Anachukua mizigo yangu kwa
siku nzuri na mbaya.
 
Sijaiona nyingine siku,
Na jana imenipita.
Na leo Mungu anayajua
hitaji yote ninayo.
 
2 Sitasumbuka kwa kuwa
Mungu ni Baba yangu kabisa.
Hawezi kunisahau mimi,
Akijificha kidogo.
 
3 Sitasumbuka kwa kuwa
Mungu ananilisha kamili.
A’nipa yote yanifaayo,
Kwa roho yangu na mwili.
 
4 Ninafurahi kwa kila saa,
Na sawa ndege 'naimba.
'Najua kweli kwa kila siku,
Baba’ngu ananipenda.